Hatimae klabu ya Man City, imethibitisha kumsajili beki kutoka nchini England John Stones akitokea Goodison Park yalipo makao makuu ya klabu ya Everton kwa ada ya Pauni milioni 47.5.

Man City wamethibitisha usajili wa beki huyo dakika chache baada ya jina la Stones kuonekana kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa UEFA, tayari kwa michuano ya ligi ya mabingwa.

Hali hiyo ilizua utata kutokana na taratibu za usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 kutokufahamika hapo awali, lakini sasa imekua rasmi.

Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Man city imeeleza kuwa, Stones amesaini mkataba wa miaka mitano.

Audio: Lissu afunguka tena kuhusu agizo la Rais Magufuli, “Mahabusu si pazuri, lakini...”
Mbowe, Lissu walimwa barua na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma