Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Rasmus Hojlund, anatarajiwa kuanza katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Denmark, Kasper Hjulmand, ameibainisha hayo baada ya kumjumuisha Mshambuliaji huyo katika kikosi chake kwa ajili ya michezo ya kufuzu Euro 2024 dhidi ya San Marino na Finland, Septemba mwaka huu.
Mshambuliaji huyo ambaye ametua Man United msimu huu kwa Pauni 72m akitokea Atalanta, hajacheza mchezo wowote kutokana na kuwa majeruhi.
Imeelezwa kuwa, huenda ikawa ngumu kwa Hojlund kuanza moja kwa moja dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili (Septemba 03), lakini uwezekano wa kukaa benchi upo.
Kocha wa Denmark, Hjulmand, alisema amezungumza na Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag juu ya Mshambuliaji huyo.
Tumewekeana makubaliano na klabu kuwa anahitaji muda wa kucheza kuona maendeleo yake kwani ameshindwa kufanya hivyo. Lakini ndani ya Denmark ataenda kucheza ingawa tutaangalia hali yake,” alisema kocha huyo wa Denmark.