Klabu ya Manchester United inatarajia kumtambulisha Mshambuliaji wake mpya, Rasmus Hojlund kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Lens utakaochezwa baadae leo Jumamosi (Agosti 05).
Timu hiyo itacheza mchezo wake wa kwanza kwenye dimba Old Trafford baada ya kutoka kwenye ziara ya kujiandaa na msinmu na itawakaribisha mashabiki wao kushuhudia mtanange huo huku wakiwa na shauku ya kumuona Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark.
Man United ilikamilisha uhamisho wa Mshambuliaji huyo baada ya kushindwa kuinasa saini ya Washambuliaji Harry Kane na Victor Osimhen kutokana na dau la wawili hao kuwa kubwa.
Mdenmark huyo alijiunga na Mashetanà Wekundu akitokea Atalanta baada ya kunasa saini ya Mason Mount, Andre Onana ambao wataongeza nguvu kwenye kikosi.
Mkongwe wa Man United, Rio Ferdinand alikuwa na mchango hadi saini ya Hojlund inapatikana kwa Pauni 72 milioni.
Mkongwe huyo alisema kuhusu uhamisho wa Hojlund: “Aina ya uchezaji wake unaendana na Ligi Kuu England na anaamini atafanya vizuri.”
Utambulisho wa Hojlund ulichelewa kutokana na kutokamilisha kibali cha kufanya kazi na VISAa ya kuishi England na kuzua hofu kwa mashabiki lakini sasa kila kitu kimekwenda sawa.
Wakati huo huo Ousmane Dembele amekamilisha uhamisho wa kwenda Paris Saint-Germain kwa Pauni 43 Milioni. Maamuzi hayo yamefanyika haraka baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano.
Winga huyo atasaini mkataba wa miaka mitano wa kukipiga PSG kwa mujibu wa mkali wa usajili Fabirizo Romano.