Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru anatarajiwa kuzikwa leo saa tisa alasiri katika makaburi ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau inaonesha kuwa jana saa 10 jioni mwili wa marehemu ulitolewa Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria /Makumbusho ambako ibada itafanyika kisha kufuatiwa na mkesha.
Ratiba Fupi ya mazishi ya Kingunge ni kama ifuatavyo
Saa 1:00-2:00 asubuhi- Waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
Saa 4:00-5:00 asubuhi- Misa nyumbani kwa marehemu
Saa 6:00-9:00 mchana kuaga mwili wa marehemu kwenye ukumbi wa Karimjee.
kisha mwili wake kupelekwa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni yaliyopo Jijini Dar Es Salaam, Mungu ailaze roho ya marehemu Kingunge Ngombare Mwiru mahali pema Peponi.
Kingunge aliaga Dunia mnamo tarehe 2, Februari 2018 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kung’atwa na mbwa mwishoni mwa mwaka jana nyumbani kwake.