Droo ya raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA imetoka huku timu za ligi kuu ya England zikipangwa na zile za madaraja ya chini.

Mabingwa watetezi Arsenal, wamepangwa kukipiga na timu ya Burnley, Huku Chelsea wao wataanzia ugenini kwa kucheza na Mshindi wa mchezo kati ya Northampton Town au Mk Dons.

Man City wao watakipiga na mshindi wa mchezo wa Wycombe Wanderers au Aston Villa. Huku majirani zao Man United wao watakipiga na Derby County.

West Ham, wanasubiri mshindi wa mchezo unaowakutanisha Exeter City dhidi ya majogoo wa Anfield Liverpool.

Michezo hii ya raundi ya nne itachezwa January 29 mpaka Februari 1.

Ratiba kamili ya raundi ya nne ya kombe la FA:

ArsenalvBurnley

Bury/Bradford CityvHull City

Carlisle United/YeovilvEverton

Colchester UnitedvTottenham/Leicester

Crystal PalacevStoke City

Derby CountyvManchester United

Eastleigh/BoltonvLeeds United

Exeter City/LiverpoolvWest Ham United

Huddersfield Town/ReadingvWalsall

Ipswich Town/PortsmouthvAFC Bournemouth

Northampton/Milton Keynes DonsvChelsea

Nottingham ForestvWatford

Oxford UnitedvNewport County/Blackburn

Shrewsbury TownvSheffield Wednesday

West Bromwich/Bristol CityvPeterborough United

Wycombe/Aston VillavManchester City

Paul Pogba Aushangaza Ulimwengu
Louis Van Gaal Achoshwa na Manchester United

Comments

comments