Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans hawatashuka dimbani katika mzunguko wa kwanza wa msimu mpya wa ligi kutokana n kukabiliwa na mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Msimu mpya wa Ligi utafunguliwa rasmi kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam tarehe 17 Agosti na kufuatiwa na mechi za raundi ya kwanza tarehe 20 Agosti.

Wakati timu 14 zikishuka dimbani wikiendi ya 20 na 21 Agosti kutupa karata zao za kwanza za msimu, Yanga inayokabiliwa na pambano la ugenini dhidi ya TP Mazembe tarehe 23 Agosti itasubiri hadi tarehe 27 kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi.

Hivyo basi, mchezo wa raundi ya kwanza wa Young African ambao utakuwa dhidi ya JKT Ruvu utachezwa tarehe 31 Agosti ikiwa ni siku nne baada ya mabingwa hao kucheza mchezo wa raundi ya pili dhidi ya African Lyon iliyopanda daraja.

Baada ya kucheza na African Lyon na JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa, Young Africans itasafiri kwenda Mtwara kucheza mechi yake ya kwanza ya ugenini dhidi ya Ndanda tarehe 7 Septemba.

Kwa upande wa mahasimu wao, Simba SC wataanza mbio za kuusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyoukosa kwa miaka minne mfululizo iliyopita kwa kuikaribisha Ndanda.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza y Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kupigwa tarehe 20 Agosti katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Mtihani wa pili wa Simba utakuwa dhidi ya maafande wa JKT Ruvu, pambano lililopangwa kupigwa tarehe 27 Agosti.

Kikosi cha kocha Omog kitaendelea kupumus katika uwanja wa Taifa katika mchezo wake wa tatu utakaokuwa dhidi ya maafande waliorejea Ligi Kuu, Ruvu Shooting tarehe 7 Septemba.

Ratiba hio ya msimu wa 2016/16 inaonesha Simba watacheza mechi sita za mwanzo katika uwanja wa Taifa ambao ni rafiku kwa vigogo wa Ligi Kuu.

Mashoga 150 wapanga kummaliza Makonda, aanza kuwashughulikia
Majaliwa Apokea Milioni 50 Kutoka NSSF, Ujenzi wa Shule Mpya Lindi