Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, atafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kati ya tarehe 03 Septemba, 2018 na tarehe 10 Septemba, 2018.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli ataweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Taarifa zaidi kuhusu ziara ya Mhe. Rais Magufuli katika mikoa husika zitatolewa na viongozi wa mikoa hiyo.

Aidha, baada ya kumaliza ziara katika mikoa hiyo Rais Magufuli anatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya katika tarehe zitakazopangwa.

Anthony Martial aanza kubembelezwa Man Utd
Shujaa wa Marekani atundika daruga rasmi