Baada ya Muna kuongea yaliyopo moyoni mwake kuhusu swala la marehemu mtoto wake na Patrick kusema ukweli juu ya baba wa mtoto wake kuwa ni Casto Dickson suala ambalo limezua mjadala mkubwa mitandaoni na kufanya kila mtu kuibuka na mtazamo wake na wengi wakisema alichofanya Muna ni makosa hakutakiwa kuzungumza kitu hadi arobaini itakapofika.

Mtazamo huo umekuwa tofauti kwa msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini Rehema Chalamila maaarufu kama Ray C ambaye alisema Muna yupo sawa kutua mzigo aliokuwa ameubeba kwa muda mrefu na sasa atakuwa huru.

Hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram alimpongeza Muna na kusema sasa kuna mzigo fulani atakuwa ameutua akisisitiza uhuru wa kuwa wazi unapokuwa unaumizwa na jambo fulani kwani maumivu ya moyo yakizidi yanaua.

”Una uhuru wa kuwa muwazi pale unapoona mambo fulani yamekuumiza au hayajakaa sawa, kuongea kunafanya nafsi yako inakaa sawa, safi Muna ninaamini kuna kamzigi flani umekatua kutoka kwenye moyo…good job”.

Wema Sepetu ahukumiwa jela
SUA yagundua mwarobaini tatizo la nguvu za kiume

Comments

comments