Siku chache baada ya kutoa nafasi kwa wanaume kutuma maombi ili aweze kuchachuja na kumpata mwanaume atakayeishi nae na kuzaa nae watoto wawili, Ray C ameamua kumuweka wazi mwanaume anaeupeleka moyo wake puta, si mwingine, ni rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta!

Kupitia instagram, jana Miss Kiuno bila mfupa alipost instagram picha ya rais huyo wa Kenya na kuandika siri yake ili kuufanya moyo wake upumue.

“Lemme tell u a lil secret about Uhuru!!!!I love this guy to death!I have had a crush on him for soooooo long!!!huwa namuota sana sana!!!!I love everything about him!His Attitude, His accent!Total Package!!” Aliandika.

Kwa bahati mbaya, mbali na kuwa chini ya himaya ya ikulu ya Kenya, Rais Kenyatta ana ndoa tayari na dini hairuhusu kuongeza mwanamke mwingine! Pole kwa Ray C japo wakati mwingine moyo hauna mipaka ya kupenda.

Huenda ikiwa ni utani tu, kwa kuwa siku chache baada post yake ya kutafuta mwanaume wa kumuoa na kuzaa nae iliyosababisha kupata zaidi ya maombi 500, Ray C alisema ule ulikuwa utani tu kwa kuwa mme mwema hatafutwi kwenye mitandao bali hutoka kwa Mungu.

#MTVMAMA Vijembe Vyatawala Pongezi Za Tuzo Ya Diamond, Dole La Kati Aliloonesha Lawasha Moto
Rick Ross Afunguliwa Mashitaka Na Mama Mtoto Wake