Ray C amepaza sauti yake kuwalilia mapromota, meneja na baadhi ya marafiki zake ambao wamemtenga baada ya kugundua amefilisika.

“Ninahangaika mwenyewe hivi sasa kwa sababu wale wote ambao nilikuwa nawaamini na kuwategemea wamenikimbia,” Ray C aliiambia Bongo5.

Alisema kuwa meneja na watayarishaji wa muziki wamemkimbia kwa sababu muziki unahitaji fedha ili kujiendesha lakini hivi sasa yeye hana pesa ya kulipia muda wa studio, kufanya video kubwa na kutangaza kazi zake.

Alisema kuwa yuko katika wakati mgumu kifedha kwa kuwa alitumia kiasi kikubwa cha fedha katika kufanya matibabu ya kurejea katika hali yake baada ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, Mwimbaji huyo alieleza kuwa hivi sasa amepata faraja baada ya wasamalia wema kumuahidi kugharamia kushuti video ya wimbo wake anaotarajia kuuachia hivi karibuni.

Madiwani Wa Ukawa Na CCM Washikana Mashati, Polisi Waingilia Kati
Mwanariadha maarufu amuoa mwanamke mwenzake