Hatimaye mwimbaji na muigizaji wa muda mrefu kutoka nchini Marekani Ray J amevunja ukimya na kuzimwaga siri zote alizozificha kwa kipindi cha zaidi ya miaka 14 tangu kuenea kwa mkanda wa ngono uliomuhusisha yeye na mwanamitindo na mjasiriamali maarufu Kim Kardashian kufuatia kuelemewa na maneno yanayoendelea kurushwa dhidi yake.
Mei 4, 2022 Ray j alidhihirisha kukasirishwa na madai ya Kim Kardashian kuhusu mkanda wao wa ngono uliovujishwa mwaka 2007 kiasi ambacho aliamua kuweka wazi kila kitu na hata kumtaja mama mzazi wa Kim, Kris Jenner kuwa ni mmoja wa wahusika wakuu katika kutekeleza suala la mkanda huo kuvuja kufuatia makubaliano ya kibiashara baina yao.
“Nimekaa kivulini kwa zaidi ya miaka 14 nikiiruhusu familia ya Kardashian kutumia jina langu, kudhalilisha jina langu, kutengeneza mabilioni ya dola kwa muongo mmoja na nusu wakizungumza juu ya mada ambayo sijawahi kuzungumza chochote juu yake” Ray J, mwenye umri wa miaka 41, alisema wakati wa mahojiano na Daily Mail.
“Sijawahi kuvujisha chochote. Sijawahi kuvujisha mkanda wa ngono maishani mwangu. Haijawahi kuvuja.” aliongeza.
Ray J alidai kuwa Kim Kardashian, 41, na mama yake mzazi Jenner mwenye umri wa miaka 66, walifahamu kila kitu kuhusu mkanda huo wa ngono kuwekwa hadharani kwa sababu walidaiwa kuhusika katika mpango huo ambapo pia J amedai kuwa hakuwa na picha zozote za wazi za uhusiano wake na Kim, licha ya kusambaa kwa taarifa hivi karibuni za kuwepo kwa video nyingine za wawili hao.
“Sijawahi kuwa na mkanda hata mmoja nyumbani kwangu, alikuwa nao yeye nyumbani kwake, daima amekuwa na kanda zote kwenye sanduku la viatu la Nike chini ya kitanda chake, hivyo ndivyo yote yalivyotokea.
Mara moja tu nilimpa wazo hilo, kama utani kidogo, ndipo alipolichukua wazo hilo, akazungumza na mama yake wakafanya uamuzi wao wenyewe na haikutoka mikononi mwangu”.
Baada ya mkanda huo wa ngono kuvujishwa na kuenea kote duniani, Ray J amedokeza kuhusu namna alivyopambana na shutuma nzito kutoka kwa watu mbali mbali kiasi cha kukosa pa kuuficha uso wake.
“Nilihisi kujiua kwa sababu unapojua kitu ni kweli na unatazama familia nzima inatengeneza himaya kutokana na uwongo ambao wameubuni, inavunja moyo na dharau kwa waburudishaji wote ambao wamekuwa waaminifu na wakweli kupitia uwezo wao”.
Mwimbaji huyo alieleza, akidai kwamba kimaisha mambo yalimbadilikia kwa kiasi kikubwa hata kupata kazi kwake ilikuwa ngumu baada ya taswira yake kuchafuliwa na mkanda huo kutokana na fikra zilizojengeka kwa jamii wakati huo.
Msanii huyo na mmiliki wa hit song ‘One Wish’ pia alikanusha madai ya kwamba Kanye West alipata mkanda wa pili wa ngono kutoka kwake mwishoni mwa mwaka jana. “Haikuwa kanda ya ngono ilikuwa ni picha nyingi, video nyingi ndogo na uthibitisho mwingi ambao tumekuwa tukizungumza kwa miaka mingi tangu kutengana kwetu” aliongeza.
Wakati wa mahojiano yake, Ray J alitoa picha zinazodaiwa kuwa za mazungumzo kati yake na Kardashian kuhusu matukio ya kipindi chake cha TV ‘Keeping Up With the Kardashians’. ambacho alisikika akizungumzia kwa uchache kuhusu furushi la picha na video nyingine chafu kuhusu wawili hao
Kardashian alifafanua kuwa alikuwa akitania, pia alijitolea kuweka taarifa inayoonyesha wazi kwamba hakuwa akijaribu kumhusisha Ray J kwenye masuala hayo kupitia kipindi hicho cha Luninga.