Gwiji wa klabu ya Arsenal  Ray Parlour, amempigia upatu meneja wa klabu ya Atletico Madrid  Diego Simeone kwa kusema anafaa kuwa mtu sahihi wa kurithi nafasi ya Arsene Wenger huko Emirates Stadium.

Wenger atasheherekea miaka 20 ya kuitumikia klabu ya Arsenal kama meneja itakapofika Septemba 22, huku mkataba wake ukitarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Mapema hii leo Parlour alihojiwa na tovuti ya talkSPORT na kueleza kwa nini amekua akiamini Simione ndio chaguo sahihi la kurithi kiti cha Wenger pale kaskazini mwa jijini London.

“Simeone, ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa ufundishaji soka na amekua mvumilivu wa mambo mengi kutokana na changamoto kadhaa ambazo hukutana nazo anapokua ndani na nje ya uwanja,”

“Naamini sifa hiyo inatosha kupewa kikosi cha Arsenal ambacho kitapaswa kuwa na mtu shupavu ambaye ataweza kuwafurahisha mashabiki wanaoipenda The Gunners ulimwenguni kote,”

“Ni mtu ambaye ninaweza kumlinganisha na mameneja wenye uwezo wa kupambana na yoyote katika soka ulimwenguni, ambao kwangu ni kama [Pep] Guardiola, [Jose] Mourinho, [Jurgen] Klopp na wote kwa sasa wanafundisha hapa England,”

Image result for Ray ParlourRay Parlour

Fununu za kuanza kusakwa kwa meneja mpya wa klabu ya Arsenal zimeanza kusikika kufuatia uwepo wa tetesi za babu Wenger kutarajiwa kukaa pembeni mara tu, mkataba wake utakapofikia kikomo.

Tayari meneja wa klabu ya Bournemouth Eddie Howe anatajwa katika kinyang’anyiro hicho, kwa kigezo cha kuwa na falsafa za ufundishaji kama ule wa Arsene Wenger ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 1996 akitokea klabu ya Nagoya Grampus Eight ya nchini Japan.

Eden Hazard Ampiga Kijembe Mourinho, Amfagilia Conte
Yaya Toure Afikiria Kuongeza Mkataba Man City