Wakati wakazi wa Loliondo wakipinga kuhama kwa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewataka watulie katika makazi yao kwakuwa amesema atafuata agizo la Waziri Mkuu na si Wizara hiyo.

Aidha, wiki iliyopita Prof. Maghembe aliagiza kutenganishwa kwa Pori Tengefu la Loliondo ili kilometa za mraba 1,500 zitumike kwa shughuli za uhifadhi na 2,500 zibaki kwa matumizi ya wananchi, hivyo kuwataka waondoke kwenye eneo hilo ifikapo machi 30 mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema kuwa wananchi wanapaswa kutulia na wasisikilize uamuzi wowote mwingine mbali na kamati yake ambayo inaendelea na majadiliano.

“Waziri Mkuu ni mtu mkubwa sana,anayeweza kutengua kauli yake ni Makamu wa Rais au Rais, Waziri Mkuu alinipa kazi ya kamati na kazi naendelea kuifanya,lazima kusikiliza kilio cha wananchi ambao nimewasikiliza kupitia kamati yangu,”amesema Gambo.

Hata hivyo Gambo amesema kuwa Loliondo ina eneo kubwa la kilomita za mraba 4,000 na yalikuja mapendekezo ya kulimega eneo hilo na kutenga Pori Tengefu la kilometa 1500.

 

Video: RC amgomea waziri, Kiini cha kufeli kidato cha 4 Dar chaanikwa
Paulo Duarte: Jose Mourinho Alichangia Kutupa Mbinu