Mkuu wa Mkoa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa wananchi ambao walishambulia msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudi Kitta wamechagua kuuawa, kwa kile alichokieleza wao walionyesha nia ya kumuua Mkuu huyo wa Wilaya.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo katika kata ya Ghana, jijini Mbeya ikiwa siku chache baada ya Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela kushambuliwa na wananchi wa Kijiji cha Mpunguti.

Amesema kuwa kwasababu walirusha mawe na walichagua kumuua Mkuu wa Wilaya (Kyela) na Kamati ya Ulinzi na Usalama nao wamechagua kuuawa.

“Nawaambieni ukweli hapa bado sijafungua kikosi kingine, tunasubiri watu waaanze tena ili tupige king’ora cha mwisho.” amesema Chalamila.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Jeromi Ngowi, alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wale wote  waliohusika na kuvamia msafara wa Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudi Kitta,  katika Kijiji cha Mpunguti wilayani humo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba1, 2019
Mbunge wa Mbeya mjini 'Sugu' afunga ndoa