Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema kuwa wakati wananchi wanaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19 kama ambavyo majeshi mbalimbali huwa yanajiandaa kupambana na aduai yeye angekuwa Spika wa bunge viboko vingetambaa bungeni.
Amesema hayo wakati akiongeo na baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe katika kikao cha kupokea na kujadili hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabuza serikali (CAG) ambapo amesema viongozi wa serikali ndio wanaotakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye vita hiyo.
”Hata juzi Bungeni wenzetu wale wapinzani wametoka nje lakini hapo hapo wanataka bunge lijadili dharula kupitisha fedha, sasa unajiuliza watajadili wakiwa wapi gesti au hotelini umeona ni akili za kitoto ningekuwa mimi ni Spika viboko vingetambaa wacha kabisa sababu hamuwezi kuendesha bunge kwa utoto” amesema Chalamila.
Marekani: athari za Covid 19 ni zaidi ya mkasa wa septemba 11