Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuhakikisha wanafuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa TMA ili kujikinga na athari za Mafuriko.

Kunenge amesema kwa sasa serikali kwa kutumia Wakala wa barabara TARURA na TANROAD inaendelea kukarabati miundombinu yote iliyoathiriwa na mvua ikiwemo barabara, mifereji, mito, umeme na miundombinu ya maji ili huduma ziweze kurejea kama awali.

Aidha, Kunenge ametoa pole kufuatia vifo vya watu 12 vilivyojitokeza kutokana na mvua ya juzi ambapo amesema mbali na vifo hivyo pia zaidi ya nyumba 800 ziliathiriwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi.

Kunenge ameeleza kuwa Kamati za maafa na vikosi vyote vinaendelea kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo, ili kukabiliana na madhara yoyote yanayoweza kutokea.

Hata hivyo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mito na mifereji kwa kuwa ndio chanzo cha mitaro kuziba na kusababisha mafuriko.

Ujerumani kuongeza mbinu mapambano ya Covid-19
Tanzania yatwaa Tuzo ya biashara