Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi ameonesha kushangazwa na madai ya kujikuta amelala kwenye makaburi mkoani Iringa, kitendo ambacho kinahusishwa na imani za kishirikina.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Hapi ameandika ujumbe ulioashiria kuwa analichukulia tukio hilo ni la mzaha ambapo aliambatananisha na picha yenye maneno yanayodai kufanyiwa kitendo hicho.

Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameamuru mtumiaji huyo wa mitandao ya Kijamii, Hilda Newton kwenda kujisalimisha kwa Mkuu wa Polisi Iringa kwa ajili ya kutoa maelezo kabla ya disemba 21 mwaka huu,

”Aliyetunga na kusambaza uzushi huu akajisalimishe yeye Mwenyewe kwa RPC Bwire Iringa kabla ya tar 21.12.2018 saa 2:00 asb. Nasikia ni Katibu wa BAVICHA,”ameandika RC Hapi katika ukurasa wake wa Twitter

Kupitia ukurasa wa twitter wa mtu ambaye alisomeka kwa jina la Hilda Newton, aliandika,”Naambiwa mwezi mmoja uliopita, alikuwa amelala nyumbani kwake ilipofika alfajiri alijikuta amelala makaburini,”

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa kwa sasa yuko likizo ya mwezi mmoja Jijini Dar es salaam, ambapo majukumu yake ameyakaimisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela.

 

 

Video: BASATA wanena kitakachoyakuta mabasi, bar zinazocheza 'Nyegezi'
Teleza azidi kuchafua hali ya hewa Kigoma

Comments

comments