Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Salum Hapi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuwaondoa watumishi wanne katika nafasi zao na kusubiri kupangiwa majukumu mengineyo

RC Hapi ametoa maagizo hayo Februari 19, 2022 akiwa katika ziara yake ya kikazi katika eneo la Sirari, Wilaya ya Tarime ili kusikiliza kero za wananchi na wafanya biashara wanaoutumia mpaka wa Sirari.

Aidha RC Hapi amesema kuwa nia na madhumu yakutoa maagizo hayo ni kuendeleza uboreshaji utendaji katika Halmashari ya Wilaya ya Tarime.

Watumishi waliondolewa ni pamoja na Mawene Daniel Mangweha Afisa Hesabu Mwandamizi, Mbuke Majura Makanyaga Afisa Biashara mwandamizi, Iddi M Baruna Afisa Ugavi Daraja la II na Alex William Ifunya Afisa Sheria Mwandamizi.

Sambamba na hayo yote RC Hapi ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime / Rorya kumkamata na kumfungulia mashtaka Mtendaji wa Kata ya Sirari Wankuru Waryuba kwa tuhuma za kula fedha za mapato ya ndani alizokasimiwa kuzikusanya na Halmashauri ya Tarime.

Ado Shaibu:Tume huru ya Uchaguzi haikwepeki
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 20, 2022