Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Taifa – NIDA, huku akiwataka Wakuu wa Wilaya wote kufanya uzinduzi huo kwenye Wilaya zao.

Uzinduzi huo, umefanyika katika kata ya Isuto iliyopo Halmashauri ya Wilaya Mbeya huku ukishuhudiwa na Viongozi mbali mbali wa Halmashauri hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini, Ackimu Sebastiani Mwalupindi.

katika uzinduzi huo, Comrade Homera pia amewasisitiza Viongozi wa Kata kuhakikisha wanagawa Vitambulisho hivyo vyote kwa wahusika kwani wananchi wamekuwa wakivisubiri kwa muda mrefu.

Hata hivyo, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwakuwapatia vitambulisho hivyo zaidi ya 360,000 katika mkoa wa Mbeya huku Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ikiongoza kupata vitambulisho vingi.

Idadi Wanawake waliofanyiwa ukatili wa kijinsia yatisha
Serikali yawekeza Trilioni 73 kwa Taasisi za Umma - Mchechu