Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali, Marco E. Gaguti ameweka wazi mikakati yake ya kuwafanya waendesha Pikipiki maarufu kama (Bodaboda) mkoani Kagera hasa katika Manispaa ya Bukoba kuwa mojawapo ya Utalii katika Mji wa Bukoba.
Ameyasema hayo mara baada ya kukutana na madereva Bodaboda hao wa Manispaa ya Bukoba na kufanya mazungumzo nao jinsi gani atahakikisha anasimamia mikakati yake ili wasafirishaji hao wafanye kazi zao kama yeye anavyotamani.
”Nimewaiteni katika mkutano huu, nia ikiwa ni kukutana nanyi na kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi zenu kwani najua kuwa kwa kipindi cha nyuma mmekuwa mkifanya kazi katika mazingira yasiyokuwa mazuri, na mkiwa na mivutano na Vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Jeshi la Polisi pale wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya Usalama Bararani.” amesema Gaguti
Aidha, ametaja mambo makuu matatu muhimu ambayo Bodaboda wanatakiwa kuyatekeleza haraka kwanza, Kuunda vikundi na kuvisajili vikundi hivyo katika maeneo yao ya kazi ili Bodaboda watambulike na kupitia vikundi hivyo wapate mikopo na elimu ya ujasiliamali.
Vilevile kupitia vikundi hivyo, Bodaboda wote wapatiwe elimu ya Usalama Barabarani, pia washiriki katika Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kagera kwani kumekuwa na tabai ya majambazi kujificha katika kazi ya kuendesha Bodaboda huku wakifanya uhalifu.
Pia mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kuanzia sasa hataki kuona au kusikia tena mivutano ya Bodaboda na Jeshi la Polisi bali wawe na mahusianao mazuri na kuwa kama mfumo anaofanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja.
-
Wakorinto wakutana uso kwa uso na viongozi wa CCM Njombe
-
DC Msafiri acharuka, awaweka kikaangoni watendaji
-
Video: Huu ni uwekezaji mkubwa, ni lazima nchi ipate mapato- Dkt. Chegeni
Kwa upande wake, Mdau wa Usalama Barabarani Mkoani Kagera, Winston Kabantega amemueleza mkuu wa mkoa kuwa biashara ya Bodaboda ilianzia Bukoba mjini na kuenea nchi nzima lakini sasa Mkoa wa Kagera haumo katika mikoa mitatu bora inayofanya vizuri katika biashara ya Bodaboda nchini.