Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafia na Vyombo vya Dola wilayani humo kuanza uchunguzi na kuchukua hatua kwa watumishi wote ambao wametumika kuzalisha hoja za ukaguzi wa mahesabu.

Amesema hayo wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kupitia na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) 2019/2020 wilayani Mafia,

Rc Kunenge amesisistiza Halmashauri hiyo kufunga hoja za ukaguzi kabla hazijafikia hatua ya kujieleza.

“Sitopenda kuona hoja zinaongezeka na kujirudia kwa mwaka ujao, pia niwasisitize kubuni vyanzo vipya vya mapato kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi” amesema Kunenge.

Amewataka watumishi kufuata utaratibu, kuheshimu sheria na kuwasilisha nyaraka za matumizi yote ya fedha ili kuepuka kuzalisha hoja.

Aweso amtumbua kigogo Sengerema
Biden kuzungumza na viongozi wa nchi 3 za Baltic