Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge ameagiza kutofanyika sherehe yoyote mkoani humo katika siku 21 za maombolezo ya kifo cha  aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakwe ambapo amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuheshimu msiba wa kiongozi huyo.

Ameongeza kuwa ”Rais Samia Suluhu, ametangaza siku 21 za maombolezo nitoe agizo katika siku hizo hakuna sherehe yoyote itakayofanyika”.

“Sisi ni waungwana tuheshimu mila na desturi zetu za watanzania huu ni msiba mkubwa hatuwezi kuwa na sherehe zikiendelea.”

Mkuu huyo wa mkoa ameelekeza vyombo vya usafiri Dar es Salaam kupeleka wananchi katika uwanja wa Uhuru ambako itafanyika shughuli ya kuaga mwili wa Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

“Ninatoa kibali kwa vyombo vyote vya usafiri kupeleka abiria uwanja wa Uhuru bila kujali njia walizosajiliwa. Kibali hiki ni cha siku mbili Machi 20 na 21, 2021,” amesema

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 20, 2021
Magufuli kuzikwa Machi 25