Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema kwa sasa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio.

Kunenge amesema kituo hicho kinaweza kuanza kutumika kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa katika hali nzuri na kusisitiza kuwa kuanza kutumika kwa stendi hiyo kutategemea na matokeo ya majaribio yaliyofanyika.

Ujenzi kituo cha mabasi Mbezi wakamilika kwa asilimia 80

Aidha RC Kunenge amesema kwa sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo hadi sasa Ujenzi umefikia zaidi ya 90%.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza kasi ili wakamilishe mradi mapema.

Fraga afanyiwa upasuaji
Sugu : Sina mamlaka ya kukabidhi ofisi