Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameruhusu kuanza kwa shughuli za biashara Kwenye Soko dogo la Kariakoo Kutokana na eneo hilo kutoathiriwa na Moto.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea sokoni hapo ambapo ametaka Wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara zao eneo la hifadhi ya Barabara ya kuingia sokoni humo waondoke ili Barabara ibaki wazi.
Aidha RC Makalla amesema kwa wakati huu ambao hali ya usalama Soko kubwa haijakaa sawa anashauri wafanyabiashara wachukuwe Mali zao na kuhamia Soko la Kisutu na Machinga Complex adi marekebisho yatakapofanyika.
Kuhusu Soko la Shimoni ambalo inaelezwa halijaathiriwa kwa kiasi kikubwa na moto RC Makalla amesema Kutokana na Mfumo wa umeme sokoni humo kuharibika ameagiza ufanyike uratibu Wafanyabiashara wakachukue bidhaa zao na kuhamia Soko la Machinga Complex na Kisutu.