Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,  Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa Manispaa iliyojitokeza kati ya Meya Manispaa ya Kinondoni,  Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo Mei 21, 2021 katika kikao cha pamoja kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa na kuwakutanisha Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Aidha RC Makalla amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wameahidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.

Viongozi hao walifarakana baada ya kuibuka kwa hoja kutoka kwa mmoja wa madiwani juu ya viongozi wa Serikali waliokamatwa hivi karibuni kwa kudaiwa kufuja fedha za makusanyo ya Serikali na kuswekwa ndani ambapo wakati akijibu hoja hizo Mkurugenzi amesema kuwa aliagiza vyombo vya ulinzi viwakamate kutokana na ubadhirifu wa fedha hizo.

Jonas Mkude shakani Simba SC
Lamine Moro kujitetea Young Africans