Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amefunga Mafunzo ya kuhitimu kwa Askari 628 wa Jeshi la Akiba mkoani humo na kutoa wito kwa Vijana hao wa Mgambo kuwa Viherehere wa kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu ili Kuimarisha ulinzi na usalama.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo RC Makalla amewaelekeza Wahitimu hao kufika ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ili wapangiwe shughuli za ulinzi kwenye kila ofisi za Mtendaji wa Mitaa ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo aliyotoa ya kila Ofisi ya Mtaa kuwa na Askari Mgambo Kufuatia kuuwawa kwa Mtendaji wa Mitaa wa Msumi.
Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza kipengele Cha kuhitimu wa Mafunzo ya Mgambo kuwa moja ya sifa za kujiunga na Jeshi la Polisi, Uhamihaji, Zimamoto na Magereza tofauti na Sasa ambapo kigezo Ni kupitia mafunzo ya JKT pekee.
Katika Mafunzo ya hayo, Askari Mgambo wamepata elimu mbalimbali ikiwemo Ukakamavu, Mbinu za kivita, Zimamoto, Uhamihaji, TAKUKURU, Usalama wa Taifa na mbinu nyinginezo za Kudhibiti uhalifu.