Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ametaja mambo manne yanayopaswa kuzingatiwa na Watendaji baada zoezi la kuwapanga vizuri wamachinga kukamilika.
Ameyasema hayo leo tarehe 3 Novemba 2021 katika kikaokazi kilichofanyika katika ukumbi wa Anatouglo ambapo ameushukuru uongozi wa wamachinga na wamachinga wote katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukubali kupangwa bila kugombana wala kusukumana ambapo zoezi hilo sasa litakuwa endelevu.
Hata hivyo Makalla amewataka Wakurugenzi wote kutekeleza suala la usafi katika maeneo yote waliyoondolewa wamachinga ili kulifanya Jiji kuwa safi muda wote.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi wote kuhakikisha katika maeneo yote waliyopangiwa wamachinga yanakuwa na huduma zote muhimu za kijamii sambamba na LATRA kupelekea huduma za Usafiri.
Vilevile Makalla amesisitiza maeneo yote waliyoondolewa machinga kulindwa, na sheria zifuate mkondo wake kwa watakaorudi katika maeneo hayo sambamba na elimu kutolewa ili wananchi wapate uelewa wa kutokufanyia biashara katika maeneo hatarishi
Amesema killa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inalo Dawati la kuwahudumia machinga hivyo wapatapo changamoto yoyote wasisite kwenda kuhudumiwa katika madawati hayo.