Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewataka Watumishi wote wanaokwenda kutekeleza na kuhakiki Kaya maskini kuhakikisha wanazingatia Weledi ili Mradi wa TASAF Kipindi Cha pili cha awamu ya Tatu kiweze kuwa na mafanikio makubwa Katika kupiga Vita Umaskini.
RC Makalla amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Semina ya kuwajengea uelewa Viongozi, Watendaji na wawezeshaji wa TASAF Wilaya ya Ilala ambapo amesema lengo la awamu hii ya Tatu ni kufikia asilimia 100.
Aidha RC Makalla amesema kumekuwa na kamchezo ka watu kuingiza majina ya watu ambao sio walengwa na kuacha wale walengwa wakitaabika Jambo ambalo ni kinyume na malengo ya Serikali hivyo ni vyema awamu hii wakahakikisha kasoro hizo Hazijirudii.
Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa Walengwa watakaopata fedha hizo kuhakikisha wanazitumia vizuri kwa kuanzisha miradi ya ujasiriamali itakayowakwamua kiuchumi huku akiwataka Madiwani kushiriki Katika kusimamia fedha hizo ili zifike kwa wahusika.