Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameagiza kuchukuliwa hatua watendaji wanaolegalega katika kusimamia maagizo yake ikiwemo ya Machinga kurejea katika Maeneo waliyoondolewa.
RC Makalla ametoa maagizo hayo alipokutana na kufanya Mazungumzo na Wakuu wa Taasisi mbalimbali, Watendaji kata, wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema baadhi ya maeneo ambayo awali yalikuwa na Biashara holela za Machinga na baadae kusafishwa yamekuwa hayasimamiwi na kusababisha Machinga kuerejea kwa wingi katika maeneo hayo huku watendaji wakishindwa kuchukua hatua.
Aidha Makalla ameyaonya Makampuni yaliyopewa dhamana ya Usafi katika Mkoa wa dsm ambapo katika Uchunguzi aliofanya alibaini kuwa kati ya Makampuni na Vikundi 256 vya Usafi ni 75 tu vinavyofanya kazi kwa Ufanisi huku vingine vikifanyakazi chini ya wastani unaotakiwa.