Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha wanaanza kuwawezesha Maafisa ugani na Ushirika wa Mkoa huo ili Waweze kutimiza majukumu yao ya kutembelea miradi ya Ushirika na sio kusota maofisini.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la nne la Ushirika Dar es salaam ambapo ametoa maelekezo sita ya kuboresha Ushirika Dar es salaam ikiwemo:-
– Kuimarisha Umoja na kuepuka Majungu, Fitina na ubaguzi.
– Kuepuka ubadhirifu wa Mali za Ushirika na kuzingatia uadilifu.
– Kuzingatia Sheria na kanuni za Ushirika.
– Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji na kuhakikisha kila wanachofanya kinawekwa Wazi kwa wanaushirika ili kuepuka majungu.
– Utoaji wa Elimu kwa wanaushirika ili wajue wajibu wao.
Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa nia yao ya dhati ya kuboresha Ushirika nchini.