Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amekutana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam ambapo ameweka utaratibu wa kufanya kikao nao kila baada ya miezi mitatu.

Makalla amesema anatambua thamani na mchango wa Wazee katika jamii hivyo ameona ni vyema kuanza majukumu yake kwa kukutana nao ili kuchota busara na baraka zao kwani anatambua Wazee ni hazina muhimu.

Aidha, amesema katika kutatua kero na changamoto za Wananchi amepanga kuanza ziara ya utatuzi Kata kwa Kata hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anayo dhamira ya dhati kuzipatia majibu kero zao.

Hata hivyo Makalla amesema kwa kuwa Mkoa wa Dar es salaam ni Mkoa mkubwa na wenye kutoa taswira ya nchi nzima kwenye kila nyanja mbalimbali, amejipanga kuhakikisha Jiji linakuwa shwari na watu wanafanya shughuli zao pasipo usumbufu wowote, kama maono na mategemeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho kwanza wamemshukuru na kumpongeza RC Makalla kwa namna anavyoheshimu Wazee na wamemuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha katika majukumu yake.

Aidha Wazee hao wamesema Wana Imani kubwa na RC Makalla kwakuwa wasifu wake wa uongozi unaonyesha kila alipopita amekuwa akiacha alama hivyo wanaamini atafanya mambo makubwa na mazuri katika Mkoa wa Dar es salaam.

Hedhi sio laana - Dkt. Gwajima
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 25, 2021