Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuwa Kutokana na changamoto ya ardhi, mkoa huo umeazimia kujenga magorofa 20 kwa ajili ya madarasa kama alivyoagiza Rais Samia.
Amesema hayo leo Machi 7, katika ziara maalum ya Rais Samia katika Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa kama iliyopo mkoani humo.
Makalla ameeleza kuwa “Kwa mkoa wa Dar es Salaam ulishatoa maelekezo ardhi haitoshi juu ya kuangalia namna ya kujenga magorofa na hata hapa tutajenga magorofa katika hosteli na kumbi za mikutano, kwa kuwa maelekezo hayo ulishayatoa,” amesema Makalla
Aidha amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Sh15 bilioni zilizowezesha ujenzi wa madarasa yapatayo 747.
Amesema uwepo wa madarasa ya kutosha kwa mwaka huu umewafanya wazazi na walezi kusheherekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya bila usumbufu wowote
Pia ameongeza kuwa uandikishaji wa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari umeongezeka na kufikia asilimia 95 kwa shule za Msingi na 94 kwa Sekondari.