Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi magari ya kisasa 18 kati ya 26 yaliyopelekwa mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu kwaajili ya kufufuliwa upya.
Magari hayo yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa yamebebwa kutokana na ubovu, lakini sasa yanarejeshwa Dar es Salaam yakiwa mazima huku yakiwa na muonekano mpya, ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba askari 11.
Akikabidhi Magari hayo kwa Jeshi la Polisi, Makonda amesema kuwa yataenda kuhudumia Wananchi kwa kuimarisha ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam, hivyo wananchi wasiwe na hofu.
Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha jeshi la polisi ni baada ya kuona Askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuawa na kuporwa Silaha.
- Kituo cha Kuwahudumia Wagonjwa wa VVU kujengwa Mererani
- Madereva wanao endesha magari mabovu Waonywa
- Lukuvi kupambana na watakaoshindwa kuwajibika
Hata hivyo, makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam, Lazaro Mambosas na viongozi wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo wamempongeza RC Makonda kwa ubunifu mkubwa alionao