Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amewaagiza maafisa wa Forodha katika kituo cha Sirari mkoani humo kuhakikisha kuwa madereva wa malori kutoka Kenya hawaingii nchini kupitia mpaka huo.

Amesema kuwa kuanzia sasa magari hayo ya mizigo yatalazimika kushusha mizigo mpakani hapo na wenye mizigo kuifaulisha katika magari ya Tanzania ili kuepuka muingiliano wa madereva kutoka Kenya na kuja nchini.

Aidha, amesema kuwa serikali ya Tanzania haina shida na maamuzi ya nchi ya Kenya kufunga mipaka yake kwavile nchi hiyo ni nchi huru yenye uwezo wa kufanya maamuzi yoyote juu ya mipaka yake na kwamba Tanzania na Kenya ni marafiki na ndugu .

Wakulima wa pamba Maswa warudishiwa fedha walizodhulumiwa
Simba SC yajitosa jumla jumla kwa Sarpong