Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amewataka watumishi wa Serikali kuacha mara moja kufanya kazi kwa mihemko ya kisiasa.
Ametoa onyo hilo wakati wa kikao na maafisa watendaji wilayani Kilolo, ambapo amesema kuwa imeibuka tabia kwa viongozi wa serikali kujihusisha na siasa wakati wa utendaji wao wa kazi.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inataka watu wafanye kazi na sio siasa kwakuwa muda huo bado haujafika hivyo kufanya siasa wakati wa kazi ni kosa kubwa.
“Haiwezekani kila siku mnafanya siasa tu, badala ya kuandaa mpango kazi wa maendeleo utakao wasaidia wananchi na kuliletea maendeleo taifa,”amesema Masenza
Hata hivyo, Masenza ameongeza kuwa kama kuna mtendaji wa serikali anataka kufanya sisa kwa sasa basi hana budi kuachia ngazi ili akashiriki vizuri shughuli za siasa akiwa huru.