Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mawnri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Maofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya zote kuhakikisha wamekamilisha zoezi la kuwatambua na kuwapatia vitambulisho vya matibabu kwa wazee wote ambao wana umri wa miaka 60 kuendelea.
Ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee Mkoani humo na baada ya takwimu za waliopatiwa vitambulisho hadi sasa kuwa kidogo wakati wazee wengi wakiwa bado hawajapatiwa.
Amesema kuwa kati ya wazee 74,454 waliotambuliwa ni 26,000 ndio wameshapata vitambulisho hivyo na kuongeza kuwa wengine bado hawajatambuliwa.
Aidha, Mwanri amesema kuwa katika zoezi hilo la kuwatambua na kuwapatia vitambalisho hakuna kumuacha mzee hata mmoja aliye na sifa kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003.
Hata hivyo, ameongeza kuwa baada ya mwezi mmoja kupita Afisa Ustawi wa Jamii ambaye atakutwa katika Halmashauri yake kuna wazee wenye sifa hawana vitambulisho ajue hana kazi.
-
Serikali yamwaga ajira 2,160 kwa walimu
-
Bei ya mifugo yapaa sokoni
-
NBS kujenga kituo kimoja cha Takwimu za Afya
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema Serikali inawategemea sana wazee hao katika kutoa ushauri ili watendaji wafanye maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.