Uongozi wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa huo Kamishna Mstaafu, Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.
Katika kuhakikihsa tukio hilo halijirudii, Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
“Nimekataza binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.
Aidha, Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.
Ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.
-
Video: RC Makonda awatembelea wagonjwa wa macho
-
Majaliwa apiga marufuku kuwekwa rumande watumishi wa umma
-
Gambo: Lema anapoteza muda wake bure
Lori hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.
Waliofariki katika ajali hiyo ni
- Domona Tenganamba, 41yrs, mfipa mkulima.
- Emmanuel Rashid 84yrs, mfipa mkulima, mkazi wa ntemba
- Restuta Sunga , 35yrs, mfipa mkazi wa ntemba
- Salula Revana 64yrs, mfipa mkazi wa mtapenda isale
- Ferisia Tenganamba , miaka 1 – 6/12
- Prisca Madeni, 45yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa china
- Richard Chikwangara, 24yrs, mfipa, mwalimu mkazi wa kalambanzite
- Yusta Somambuto, 36yrs, mfipa, mkulima mkazi wa kizumbi
- Gilesi Ramadhan, 24yrs, mfipa, mkulima mkazi wa sumbawanga
- Odetha Madirisha 46yrs, mfipa mkulima wa kizumbi
- Megi Nalunguli, 52yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
- Abuu Amani @ mandevu, 37yrs, muha, biashara, mkazi wa liapinda
- Nyandindi Batrahamu, 35yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa sumbawanga
- Magdalena Mbalamwezi, 50yrs, mfipa, mkulima mkazi wa ntuchi
- Mtoto mchanga wa wiki mbili, mwanaume ambaye hajapewa jina
Majeruhi wa ajali hiyo ni:-
- Dismas Clement, 26yrs, mfipa, mkulima mkazi wa mwinza
- Sema Savery 25yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
- Ally Haruna, 33yrs, mfipa, mkazi wa namanyere
- Yusta Mfundimwa, 50yrs, mkulima mkazi wa izinga
- Tenesfory Oscar, 36yrs, mfipa mkazi wa wampembe
- Amos Kitambale, 25yrs, mfipa, mkazi wa wampembe
- Neema Mwanandenje, 21yrs, mfipa, mkazi wa mlambo
- Joseph Sungula, 28yrs, mfipa, mkulima.
- Majeruhi mmoja mwanamke ambaye hajafahamika kwa jina yuko icu
Hata hivyo, Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka lakini juduhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea kufanyika