Katika kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali kwaajili ya ukarabati wa shule mbalimbali Kongwe zinatumika ipasavyo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu, Zelote Stephen amewataka wale wote wanaohusika na usimamizi wa fedha za ukarabati wa moja ya shule Kongwe nchini, kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kama zilivyokusudiwa.
Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea maeneo yote ya shule yanayoendelea kukarabatiwa kujionea hatua waliyofikia katika ujenzi na kutathmini kama thamani ya pesa inakwenda sambamba na ujenzi unaoendelea katika shule hiyo.
Aidha, Shule ya Sekondari ya Kantalamba ni miongoni mwa shule kongwe 20 nchini ambazo Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeweka mpango wa kukarabati shule hizo kwa lengo la kutunza hadhi na kuziboresha zaidi. Ambapo shule hiyo imepata mgawo wa shilingi 1,123,353,700/=
“Tafadhalini sana Mwalimu Mkuu, Mkurugenzi, Afisa Elimu na sisi wote tuhakikishe kwamba shule hii imebadilika kwa kuwa hizi pesa si kidogo, bilioni sio hela kidogo, zisichezewe, zifanye kazi iliyokususdiwa na kazi yenyewe ioneshe sura ya bilioni, isijekutokea tukapata kazi nyingine ya kusema kwamba hizi pesa kazi iliyofanyika ni ya hovyo hovyo,” Amesema Zelote.
-
Mpina apiga marufuku uchimbaji na uchotaji mchanga jijini Dar
-
Prof. Mbarawa: wananchi waliopisha ujenzi wa barabara watalipwa kwa mujibu wa sheria
-
Jafo ang’aka, awataka maafisa elimu kuboresha mazingira ya shule nchini
Vile vile, mara baada ya kujionea juhudi zinazoendelea katika ukatabati huo ameusifu uongozi wa shule kwa kuajiri mafundi vijana waliopo mtaani ili kuwa na matumizi mazuri ya fedha hizo tofauti na kuwatumia wakandarasi ambao wangesababisha fedha nyingine zipotee bila ya sababu.
Hata hivyo, amesisitiza kuwepo kwa uwazi kwenye matumizi ya fedha za umma, na kuwataka wakaguzi kuwa makini na kukagua kila hatua ya ujenzi na kuona kuwa kila senti inayotumika inaendana na thamani ya ujenzi inayoonekana