Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameziagiza halmashauri nne za mkoa huo kushirikiana na Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO kuhakikisha wanakuwa na viwanda vipya 25 hadi kufikia Disemba mwaka 2018 ili kutimiza agizo la serikali la kuwa na viwanda 100 vipya kwa kila Mkoa.

Amesema kuwa SIDO ndio msaada mkubwa wa kuhakikisha kuwa ndoto hii inatimia kwani shirikia hilo limejaa wataalamu lakini pia hutoa mafunzo ya viwanda vidogo na vya kati kwa wajasiliamali hivyo hawana budi kuwa nao karibu.

“Serikali imekwishaagiza tuwe na viwanda 100 hadi kufikia Disemba mwaka 2018 na kwa mahesabu ya haraka mkoa una Halmashauri nne, 100 ukigawa kwa nne ni 25, kwahiyo hadi kufikia Disemba 2018 kila Halmashauri iwe na viwanda hivyo vipya, na msaada upo kuna SIDO hapo ambao wataalamu wamejaa na wanatoa mafunzo kila siku ya viwanda vidogo na vya kati watawasadidia na mimi nitalisismamia,” amesema Wangabo.

Ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya diwani wa kata ya Mtowisa Mh. Edgar Malini. alipomkabidhi Mh. Wangabo Skafu iliyotengenezwa na kilichokuwa kiwanda cha nguo katika kata hiyo ambacho kilifungwa miaka zaidi ya 30 na kubaki majengo.

Hata hivyo, kwa sasa Mkoa wa Rukwa una jumla ya viwanda 950 huku kukiwa na kiwanda kikubwa kimoja, viwanda vya kati 2 na viwanda vidogo 947.

 

TFF kula sahani moja na waliosambaza ujumbe batili
Majaliwa ampa neno Dkt. Kigwangalla