Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela ametoa miezi miwili kwa madiwani mkoani humo kuhakikisha wanayatambua maeneo ya Vijiji yaliyogawiwa kwa wawekezaji bila kufuata sheria kuanzia ekari 50 kwenda juu ili yarejeshwe kwa wananchi na yatumike kwajili ya shughuli za kimaendeleo.

Shigela ametoa agizo hilo wakati akifungua semina elekezi ya Utawala bora na utatuzi wa migogoro ya kisheria kwa madiwani wa Mkoa huo.

Amesema kuwa kumekuwepo na migogoro ya Ardhi katika maeneo ya vijiji iliyotokana na baadhi ya viongozi wa sio waadilifu waliotumia dhana zao walizopewa vibaya na hivyo kugawa maeneo makubwa ya Ardhi kwa watu wachache.

“Natoa miezi miwili kwa Madiwani nendeni mkawasimamie Wenyeviti wa vitongoji na vijiji kubainisha maeneo yote ya Ardhi ambayo yamegaiwa isivyo halali na kusababisha wananchi kukosa maeneo ya kufanya shughuli za uzalishaji” amesema RC Shigela.

Magufuli aibana Wizara ya Afya
Serikali kula sahani moja na wanaodhalilisha walemavu