Serikali Mkoani Tabora imeagiza kukamata wazazi au walezi ambao hadi kufikia Jumatatu ijayo 15January 2018 watakuwa hawajawapeleka watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule walizochaguliwa.
Agizo hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afisa Elimu Mkoa iliyoakuwa ikionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2018 bado hawajaripoti katika Shule walizopangiwa.
-
Mrema afungua kesi rasmi dhidi ya kuzushiwa kifo
-
Serikali yatoa agizo zito shule binafsi, mwisho 20/1/2018.
-
TLS yaeleza mamilioni yaliyokusanywa gharama za matibabu Lissu
Amesema kuwa kufikia Jumatatu ijayo anataka kupata taarifa na majina ya wanafunzi wote waliochaguliwa nab ado hawajaripoti shuleni ikiwa na majina ya wazazi wao ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa kwa kosa la kumkoshesha watoto haki ya kupata elimu.
Mwanri aliongeza kuwa viongozi wa kuanzia mitaa, vitongoji, vijiji , Kata na Wilaya ni vema wahakikishe wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa ambao hawako shuleni ili kujua walipo na wanafanya nini kwa kuwa inawezekana wapo ambao tayari wameshaozeshwa.
“Hapa tutakwenda kwa Sera ya mbanano kama kiongozi lazima umbane mzazi ambaye hadi hivi sasa hajampeleka mtoto shule wakati wenzake wameshaanza masomo na ikibidi mfikisheni katika vyombo vya Sheria ili ajibu mashitaka yake ya kunyima mtoto haki yake ya elima”alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora.