Klabu ya Real Madrid imepanga kuanza mazungumzo na Bayern Munich ili kuipata huduma ya beki wa timu hiyo, Alphonso Davies, kwenye dirisha lijalo.

Madrid inataka huduma ya beki huyo kwa sababu inaamini ataenda kuwa mbadala wa Marcello kwenye beki wa pembeni.

Beki huyu mwenye umri wa miaka 22 wa Timu ya Taifa ya Canada licha ya kupewa ofa ya kusaini mkataba mpya alikataa kufanya hivyo jambo linalotoa ishara kwamba anafikiria kuondoka.

Hata hivyo, Madrid haijahusika hata kidogo kwenye suala la staa huyo kugoma kusaini mkataba mpya na Munich bado haijakata tamaa ya kumsainisha.

Davies ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Bayern na amekuwa akisifika kwa uwezo wake ambao umefanya apewe jina la utani la pikipiki.

Madrid ipo kwenye mpango wa kutengeneza kikosi kwa wachezajį wengi vijana na umri wa Davies unaonekana kuwa sahihi kwao.

Aubin Kramo kurudi nyumbani Ivory Coast
Rais Samia mjumbe Bodi ya ushauri Kituo cha Dunia