Inaelezwa kuwa Mabingwa wa Soka Barani Ulaya Real Madrid watavunja rekodi ya Dunia ya usajili endapo itawanasa Kylian Mbappe na Jude Bellingham wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Mshambuliaji wa PSG, Mbappe mwenye umri wa miaka 24 aliyesaini mkataba wa miaka mitatu na miamba hiyo ya Ufaransa, ataingiza Pauni 547 milioni, lakini sasa Madrid imeanza upya mipango yao ya kumnasa.

Madrid ilionyesha nia ya kumsajili Mbappe tangu mwaka 2021 lakini ofa yao ya Pauni 154 milioni ilipigwa chini na PSG, lakini haikuta tamaa licha ya kumpotezea kimtindo baada ya kushindwa kumsajili.

Hivi karibuni fowadi huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliweka wazi ana furaha kukipiga PSG na hana mpango wa kuondoka kwenye klabu hiyo.

“Kwangu kucheza hapa (PSG) najivunia mno, niliwasili hapa tangu nilipokuwa mdogo, nimekulia hapa na sasa nimekua mtu mzima nje na ndani ya uwanja, sidhani kama nitaondoka, sitaki kuikosea heshima klabu, nipo hapa na nina furaha, sifikirii kuhusu kitu kingine chochote kwasasa,” amesema Mbappe

Taarifa iliyotolewa juma lililopita ni kwamba Madrid ilizungumza na Borussia Dortmund kwaajili ya Jude Bellingham, ikaelezwa kiungo huyo yupo mbioni kusajiliwa na atakuwa mchezaji wa pili duniani atakayekuwa akilipwa mkwanja mrefu.

Norway yataka idadi kubwa ya wanawake viongozi
Ajali ya Wanafunzi: Serikali kugharamia matibabu, mazishi