Meneja wa klabu  ya Real Madrid imesema itakata rufaa kupinga hatua ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), kuipa kifungo cha kutosajili kwa vipindi viwili vijavyo.

Madrid wamekumbana na adhabu hiyo baada ya kubainika kutenda kosa la kusajili wachezaji walio chini ya umri, hivyo kukiuka kanuni na masharti ya FIFA.

Akizungumzia sakata hilo, meneja wa sasa wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema, hatua ya ukataji rufaa ameiacha mikononi mwa uongozi wa rais Perez ambaye ndiye atakayefuatilia kwa karibu suala la kupangua adhabu hiyo.

“Rais Perez atalisimamia suala zima la adhabu yetu kwa sababu litatuathiri kwa kiasi kikubwa. Ndio maana tumeweka azimio la kukata rufaa,” alisema Zidane.

Adhabu hii ya Madrid inafanana na ile ya mahasimu wao, Balcelona ya mwaka 2015.

Real Madrid na Atleteco Madrid wamekutwa na hatia ya kusajili wachezaji walio chini ya umri usioruhusiwa na matokeo yake wamepigwa marufuku kusajili wachezaji au kuuza kwa vipindi viwili vijavyo.

Hata hivyo, Real Madrid wanaweza kusajili wachezaji lakini hawatoweza kucheza mpaka muda wa kifungo kumalizika, itakuwa kama ilivyokuwa kwa Arda Turan, ambaye alisajiliwa na Balcelona msimu uliopita lakini ilibidi kusubiri hadi kipindi cha kifungo cha kiishe.

Katika upande mwingine, imefahamika kwamba watoto wane wa kocha wa Madrid, Zinedine Zidane walikuwa wamejumuishwa katika listi ya FIFA ya wachezaji waliosajiliwa kinyume na sheria na Real Madrid.

FC Bayern Munich Watupa Jicho Hispania
Tanzia: Mwandishi wa 'Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe' afariki