Mshambuliaji kutoka nchini Wales Gareth Bale, amekubalia kusaini mkataba wa miaka sita wa kuendelea kuitumikia klabu ya Real Madrid.

Asubihi hii kituo cha redio cha Cadena Ser kilichopo mjini Madrid kimeripotiwa kuwa, Bale atasaini mkataba wa miaka sita wakati wowote kuanzia sasa baada ya mazungumzo ya awali yaliyowahusisha viongozi wa Real Madrid kufanikiwa kwa asilimia 100.

Kimahesabu mshambuliaji huyo aliyejiunga na Real Madrid kwa ada iliyoweka rekodi duniani ya Euro milioni 100 mwaka 2013, atakuwepo klabuni hapo hadi 2022.

Kituo hicho cha redio pia kimeripoti kuwa, Cristiano Ronaldo, Pepe pamoja na Luka Modric nao wanajiandaa kuingia katika mpango wa kusainishwa mikataba mpya ya kuendelea kuitumikia Real Madrid.

Beki wa kati kutoka nchini Ureno Pepe, anajiandaa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Ronaldo, ambaye anashikilia rekodi ya ufungaji bora kwa wakati wote wa Real Madrid anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne huku Luka Modric akijipanga kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Uongozi wa Real Madrid umeibuka na mkakati wa kuwasainisha baadhi ya wachezaji wao mikataba mipya, kufuatia rungu la adhabu lililoangushwa na FIFA ambalo linawanyima nafasi ya kufanya usajili katika vipindi viwili vya usajili.

FIFA wameiadhibu Real Madrid baada ya kubaini waliwahi kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni ambao walikua chini ya umri unatambulika kisheria.

Jordan Henderson: Southgate Astahili Kukabidhiwa Kijiti
Vincent Bossou: Adebayor Ataniondoa Young Africans