Shirikisho la soka duniani FIFA, limeziadhibu klabu ya mjini Madrid nchini Hispania, Real Madrid na Atletico baada ya kufanya usajili wa wachezaji vijana kinyume na utaratibu.

FIFA wamezifungia klabu hizo, kusajili wachezaji hadi mwaka 2017 pamoja na kuzitoza faini.

Kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo lenye mamlaka ya soka ulimwenguni kote, ilikutana na imebaini kuna makossa yalifanywa kwa makusudi na viongozi wa klabu hizo mbili, katika usajili wa wachezaji chini ya umri wa miaka 18.

Real Madrid wametozwa faini ya paund 622,000, huku Atletico akitozwa faini ya paund 248,000.

Hata hivyo klabu hizo zinaruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

Adhabu ya kufungiwa kusajili itaanza katika msimu wa majira ya kiangazi ambao utaanza mwishoni mwa msimu wa 2015-16.

Startimes Raundi Ya 11 Kuendelea Wikiendi Hii
Mohamed Elneny Katika Muonekano Wa Kiarsenal