Klabu ya Real Madrid imeanza mazungumzo na uongozi wa AS Monaco ya Ufaransa kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa usajili wa kiungo Bernardo Silva mwishoni mwa msimu huu.

Jarida la Le 10 Sport limeandika, Real Madrid wamepitia kwa wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendez hadi kufikia lengo la kuzungumza na uongozi wa AS Monaco.

Silva ni miongoni mwa wachezaji wanaopagawisha soka la barani Ulaya kwa sasa, na tayari klabu kama Man Utd imehusishwa na mpango wa kumuwania.

Hata hivyo, mpango wa Man Utd huenda ukaingia shubiri kutokana na mazungumzo yanayoendelea kati ya AS Monaco na Real Madrid.

Thamani ya usajili wa kiungo huyo tayari imeshawekwa hadharani na uongozi wa AS Monaco kuwa ni Euro milioni 50.

Mwenyekiti, Katibu Chadema Lindi watoka Gerezani
'Sitakubali wakina mama wapoteze watoto wao kwa dawa za kulevya' - Makonda