Klabu ya ​Real Madrid imetangaza katika tovuti yake kuwa mshambuliaji wao wa zamani  Alvaro Morata atajiunga nao msimu huu utakaoanza mwezi Agosti.

Morata  anayeitumikia Juventus ya Italia alikuwa akiwindwa na Chelsea pamoja na Arsenal huku Juventus ambayo alijiunganayo mwaka 2014 kwa paundi 20 milioni ikiwa inamhitaji abakie.

Morata alifunga magoli 12 na kuisaidia upatikanaji wa mengine tisa katika michuano yote ya Serie A huku akicheka na nyavu mara mbili katika michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa.

Mkurugenzi mtendaji wa Juventus Giuseppe Marotta mapema wiki hii alinukuliwa akisema wanatarajia kupokea ofa toka Madrid siku chache zijazajo.

“Tunategemea kupokea ofa kwa maandishi siku zijazo kwa mchezaji wetu na kuna asilimia chache sana za kuendelea kubaki nasi msimu ujao” alisema Morotta.

Madrid walimuuza Morata kwa Juventus huku wakiweka kipengele cha kupewa kipaumbele kama watahitaji kumnunua tena.

Simba Kuanza Mazoezi Chini Ya Jackson Mayanja
Waziri Mpango Awataka (TCRA,TRA na BOT) Kushirikiana.