Uongozi wa klabu ya Inter Milan umejipanga kuanza mazungumzo na mshambuliaji kutoka nchini Argentina Mauro Icardi, ili kukamilisha hatua ya kumsainisha mkataba mpya.
Mpango huo umeibuka kufuatia tetesi zinazoendelea, kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo kulazimisha kuondoka mwishoni mwa msimu huu, na tayari klabu ya Real Madrid inatajwa kuhusisika na mikakati ya kumsajili.
Mkataba wa sasa wa Icardi ambaye ni nahodha wa kikosi cha Inter Milan, utafikia kikomo mwaka 2019.
Inter Milan wamepanga kumsainisha mkataba wa miaka miwili, ambao huenda ukamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2021, huku kiasi cha Euro milioni 110 kikitengwa kama mshahara.
- Kweli Arsenal wana mkosi, Sanchez aumia tena
-
Kocha wa Hard Rock ataja sababu za kubamizwa na Simba SC
Hata hivyo mpaka sasa wakala wa Icardi hajazungumza lolote kuhusu uwezekano wa mchezaji wake kukubali ama kukataa kusaini mkataba huo.
Icardi alianza kuitumikia Inter Milan mwaka 2013, baada ya kusajiliwa akitokea Sampdoria, na tayari ameshacheza michezo 127 na kufunga mabao 77.