Mabingwa wa Ulaya Real Madrid imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuiondoa Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya magoli 4-3.
Katika mchezo huo, Real Madrid ilikuwa inahitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kutinga fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa upande wa vilabu barani Ulaya.
Aidha, alikuwa ni Joshua Kimmich alianza kufunga goli la mapema katika kipindi cha kwanza kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Madrid baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Marcelo.
Makosa ya mlinda mlango wa Bayern, Sven Ulreich yaliizawadia Madrid goli la pili lililopachikwa na Benzema kabla ya James Rodriguez kusawazisha.
Hata hivyo, Real itakumbana na Liverpool ama Roma katika fainali itakayopigwa jijini Kiev, Ukraine May 26 mwaka huu.
-
Zinedine Zidane: Tutashambulia mwanzo mwisho
-
Eusebio Di Francesco: Tutaishangaza tena dunia
-
Jurgen Klopp athibitisha kurejea kwa Adam David Lallana